Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe akipokewa na mkuu wa kitengo cha Kuboresha usalama wa jamii ( DCP) Godluck Mongi alipokwenda kufungua mafunzo ya upelelezi kwa askari wa polisi 100. ( katika ni Mkuu wa mafunzo wa Jeshi la Polisi DCP Ally Lugendo. Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha polisi kidatu yamefadhiliwa na Taasisi ya Hanns Sidel.
………………..
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe amefungua mafunzo ya upelelezi kwa askari 100 kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni, mkoa ambao Jeshi la polisi nchini limeuchangua kuwa eneo la mfano katika kutekeleza mpango wa kuboresha usalama wa jamii uliozinduliwa katika viwanja vya Biafra kinondoni jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo ya upelelezi ya miezi miwili yamefunguliwa katika chuo cha maafisa wa Polisi kidatu kilichopo mkoani morogoro yamefadhiliwa na taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Hanns Sidel inayotekeleza miradi mbalimbali hapa nchini.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa huo, Dkt Kebwe alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha cha Jeshi la Polisi kuamua kuchangua mkoa wa Morogoro kufanyia mafunzo hayo na pia kumchagua yeye kuwa mgeni rasmi.
Dkt Kabwe alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi ngumu wanayoifanya ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao na aliwataka askari wanaopata mafunzo hayo katika chuo cha maafisa wa polisi kidatu kutumia weledi na taaluma hiyo watakayoipta kutatua kero za wananchi zinazotokana na ucheleweshaji wa upelelezi .
“ Nimefurahi sana kusikia kuwa mafunzo haya yanalenga kuharakisha upelelezi na kesi yoyote itakuwa inapelelezwa itakuwa imekamilika ndani ya siku sitini” alisema Dkt Kebwe.
Mapema akitoa utangulizi wa mafunzo hayo, mkuu wa kitengo cha kinachoratibu utekelezwaji wa mpango wa Jeshi la Polisi wa kuboresha usalama wa jamii, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Godluck Mongi alisema kuwa mafunzo hayo ya upelelezi yataleta mafanikio makubwa katika mkoa huo wa kinondoni kwa kuharakisha upelelezi wa kesi .
Aliongeza kuwa lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 askari wote upelelezi wawe wamepata mafunzo hayo na hatimaye kupuza kero ya uhalifu katika mkoa wa kinondoni kwa asilimia 10%
Naye mwakilishi wa Taasisi inayofadhili mafunzo hayo, Bw. Ombeni mhina alisema kuwa ufadhili wa mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi 100 kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni ni sehemu ya mpango wa Taasisi ya Hanns Seidel kuunga mkono jitihata za jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwa raia na mali zao kupitia mpango wa kuboresha usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi kinondoni.
Aliongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi sitini ambazo jumla ya miradi 100 inaendelea kutekelezwa ikiwa na lengo la kukuza demokrasia, amani na maendeleo duniani kote.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrea Mwang’onda aliwataka wanafunzi wanaopata mafunzo hayo ya upelelezi kuzingatia kile wanachofundishwa na kufuata maadili yote ya uaskari wakati wote watakapokuwa katika mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment