• Breaking News

    Friday, 5 June 2015

    VITA YA BECKHAM ILIVYOIPA UTAJIRI REAL MADRID

    Na
       NIHZRATH NTANI


      Ligi mbalimbali barani ulaya zimemalizika. Bila shaka ni wakati mzuri kuwakumbusha  mashabiki wa soka na wapenzi wa mtandao huu, hata hivyo makala  hii haikuja tu kwenye ndoto, rafiki yangu mmoja aliniuliza swali hili  " Kwanini Ronaldinho Gaucho hakucheza Real Madrid wakati alikuwa staa kweli kweli na wakati tulikuwa na nafasi kubwa ya kumsajili  mwaka 2003, badala yake wakamsajili David Bekham?" Hakika lilikuwa swali zuri, swali ambalo lilinifanya nirejeshe nyuma kumbukumbu zangu mpaka mwaka 2003.

    David  Bekham aliwasili Real Madrid mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka 2003 akitokea Manchester United,  na kusaini mkataba wa miaka minne kuichezea 'Los Blanco' Mzaliwa huyo wa mji wa Leytonstone-London nchini Uingereza alicheza miaka minne Santiago Bernabeu. Ni usajili huu ambao uliongeza chuki ya watu wa Barcelona dhidi ya Real Madrid.

          Mwaka 2003 kulikuwa na uchaguzi wa Rais wa Barcelona baada ya Joan Gaspart kujiuzulu, uchaguzi ulipangwa kufanyika mwezi juni 15, Mtu mmoja aliyeitwa Luis Bassat alikuwa anaelekea kushinda katika uchaguzi ule, alikuwa mahiri  sana  kuzinadi sera zake wakati wa kampeni, na kujikuta akipata uungwaji mkono wa wanachama wengi wa Barcelona.

          Mgombea mmoja wa Urais aliyeitwa Joan Laporta, aliubadili upepo ule baada ya kuja na sera ya kusema kuwa akishinda atamsaini Bekham, na alitangaza  kwa mbwembwe mwanzoni mwa Juni kuwa makubaliano ya kumsajili Bekham yalikuwa yamekwisha hafikiwa. Ushindi ukabakia mikononi mwake.Raha ilioje!

    Msimu wa 2003/2004, baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili ilionekana wazi kuwa Manchester United inamuuza Bekham kwenda Barca, na klabu hizi mbili zilikwisha kukubalina usajili wa Bekham kwenda Barcelona. Kuna mwanadamu mmoja anayeitwa Florentino Perez inawezekana ndie mwanadamu pekee anayechukiwa na mashabiki wa Barcelona kwa sasa ukimuondoa Luis Figo, alikuja kuharibu usajili huu, Perez aliwasiliana na Peter Kenyon aliyekuwa mtendaji mkuu wa Manchester united kuzungumza kumsaini Bekham, akaambiwa tayari makubaliano yamekwisha fikiwa.

        Mwanaume huyu akukata tamaa, akazungumza na Tony Stephen ambaye alikuwa wakala wa Bekham, Tony akamjibu Perez, Bekham hakupendezwa kuuzwa kama mzigo, hivyo anapinga makubaliano hayo, na yuko tayari kucheza Real Madrid, bado makubaliano binafsi hayajafikiwa, nafasi ya Bekham kwenda Los Blanco ipo, Mwanaume akaingia kazini .
     
       Kumbuka kuwa Manchester United walikuwa tayari wamemtafuta mbadala wa Bekham, na walikuwa katika hatua ya mwisho kumsaini Ronaldinho Gaucho kutoka PSG, na walikuwa wanamtaka kwa udi na uvumba, kipindi hicho Gaucho alikuwa nyota kweli kweli, akiwa na miaka 23, tayari alikuwa anatawala vyombo vya habari na ni Man United pekee ndio iliyopeleka ofa ya paundi 25 kumsajili.

        Perez akagundua hitaji la Man United kwa Gaucho, Real Madrid haraka wakapeleka ofa kwa Gaucho kupitia kwa wakala wake na rais wa PSG, paundi 30milioni zilikuwa mezani, upepo ukageuka Ronaldinho akavutiwa na ofa yetu, kumbuka alikuwa na marafiki pale Los Blanco wakiwemo Roberto Carlos na Ronaldo De Lima, ilikuwa ofa yenye kuvutia, Kuona hivyo Manchester United wakabakia wamefadhaika, Bekham wanamuuza Barcelona, na Gaucho wanamkosa.
          Peter Kenyon akawasiliana na Real Madrid wakiomba kuwa wako tayari kuwauzia Bekham kwa sharti ya kujitoa kumsajili Gaucho. Hilo ndio ambalo alilihitaji Perez, hakika Madrid hawakuwa wakimuhitaji Gaucho, walimuhitaji  zaidi Bekham kwa ajili ya kufanya biashara, walitaka mtu ambaye ataifanya klabu ifuatiliwe na vyombo vya habari kila wakifanyacho,  walimuhitaji mtu ambaye atakuwa maridani sana nje ya uwanja, mtu ambaye atauza jezi kupitia jina lake, mtu ambaye atavutia wadhamini wakubwa, Bekham kwa wakati ule ndie alikuwa chaguo halisi la hitaji la Los Blanco.Kwa mbinu hiyo wakafanikiwa hatimaye Bekham akauzwa Real Madrid kwa euro 35 milioni kwa mkataba wa miaka minne.

    Kwanini Manchester United walimuuza Bekham Madrid badala ya kung'ang'ania makubaliano yao na Barcelona? Machester walitambua wazi wasingeweza kushindana na Real Madrid katika kumuwania Ronaldihno, na wakajua wazi kuwa ikiwa Real Madrid wakijitoa hakuna klabu nyingine itakayoweza kushindana nao. Ni julai 1 mkataba wa Bekham ulikuja kukamilika na kumfanya David kuwa mwingereza wa tatu kuichezea Real Madrid baada ya Laurie Cunningham na Steve Mcmanaman.
          Kusajiliwa kwa Bekham kwenda Real madrid kuliwaumiza sana Barcelona hasa Laporta na mshirika wake Sandro Rosell waliona wamedhalilishwa, Wakajibu mapigo kwa Manchester United, nao wakajiunga katika mbio za kumsajili Ronaldinho, ikiwa yamebakia masaa 11 kabla ya manchester united kushinda mbio za kumtwaa Gaucho. Barcelona wakapeleka ofa ya  euro 30 milioni, ushawishi na ukaribu wa Sandro Rosell aliyekuwa makamu wa rais kipindi hicho ulisaidia, na kuiacha manchester united ikiduwaa, Usajili wa Gaucho kwenda Barcelona uliwaumiza sana mashabiki wa Manchester united. Hakika Barca hawakumuhitaji Gaucho, walifanya vile kama kisasi . Hata hivyo ni Gaucho aliyekuja kuiokoa Barcelona iliyokuwa dhoofu katika La liga, Kupitia miguu yake akaifufua Barcelona.

    Pamoja na yote hayo, Real Madrid ilifaidika na Bekham, alitambulishwa Julai 2  Santiago Bernabeu, na masaa saba baadae jezi 8000 zenye jina la Bekham ziliuzwa kwa wapenzi wa Real Madrid, Ilikuwa rekodi ya klabu, mpaka ilipokuja kuvunjwa na Cristiano Ronaldo mwaka 2009. Beckham aliondoka Real Madrid mwaka 2007, baada ya kutwaa ubingwa wa La Liga na kuiingizia klabu Dola 600 milioni. Tangu hapo tumekuwa klabu tajiri zaidi Duniani tangu mwaka 2004 mpaka leo.

    No comments:

    Post a Comment