Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Rashid Mfaume Taka (aliyesimama) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(pili kulia) ili kuongea na watumishi wa Taasisi za Serikali zinazotoa hudma katika Wilaya ya Ngorongoro.
Kamati ya Ulinzi na Usalama, wafanyakazi wa Halmashauri na Taasisi za Serikali zinazotoa huduma katika Wilaya ya Ngorngoro wakiwa katika Kikao maalum na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika Wilaya Wilaya hiyo. Katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha amewasimamisha Kazi Mwekahazina, Mwanasheria na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri kwa matumizi mabaya ya Fedh
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Ndg. Rafael Siumbu akijibu hoja wakati wa Kikao cha watumishi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mwananchi na mdau wa Maendeleo wa Kata ya Loliondo James Ndagarisho akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisgo Gambo wakati wa Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata hiyo.
Kaimu Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Ngorongoro Bi. Angela Steven akijibu kero za wananchi wa Wilaya hiyo kuhusu wahamiaji haramu na hatua zilizochukuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa Kata ya Loliondo kwenye Mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Kikazi katika Wilaya hiyo.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ameagiza maafisa watendaji wa Kata kutohudhuria viakao vya Baraza la Madiwani kwa kuwa sio wajumbe halali wa kikao hicho na fedha za posho zinazotumika kuwalipa ziende kwenye utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Rc Gambo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya Kikazi katika Wilaya hiyo ambayo ameianza mapema wiki hii. Akiongea na wananchi wa Kata ya Ngarasero alisema haoni umuhimu wa watendaji hao kuhudhuria vikao hivyo kwa kuwa wenyeviti wa Kamati za maendeleo za Kata ambao ni madiwani ndio wanaowakilisha wananchi wa Kata husika kwa mujibu wa Sheria hivyo ndio wanaopaswa kuhudhuria vikao hivyo.
Alisema “Haiwezekani kila mtu akahudhuria Vikao vya Halmashauri na kulipwa posho, haya ni matumizi mabaya ya Fedha za wananchi, kwa sababu mpaka sasa tangu Baraza la Madiwani wa Ngorongoro waazimie Maafisi hawa wahudhurie Vikao vya Baraza zaidi ya Tsh Mil 132 zimetumika kuwalipa posho maafisa hao”
Hizo ni fedha nyingi sana ambazo mngezipeleka kwenye huduma ya Afya mngeweza kukarabati Zahanati na kuipandisha hadhi kuwa kituoa cha Afya ambacho kinatoa na huduma za upasuaji kwa kina mama, sasa kuanzia leo madiwani pekee na watendaji wanaohusika kwa mujibu wa sheria ndio watakaokuwa wanahudhuria vikao hivyo ila watendaji wa Kata wabakie kwenye kata wasimamie shughui za maendeleo aliongeza.
Akiwasilisha taarifa ya Wilaya Mkuu wa Wilaya Mhe. Rashid Mfaume Taka alielezea kero za muda mrefu katika Wilaya hiyo kuwa ni pamoja na miundombinu ya barabara, mawasiliano, huduma za Afya kutokuwafikia wananchi wote, Uhaba wa walimu, madawati pamoja na huduma za Maji.
Alisema changamoto hizi zimekuwa zikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa Ngorongoro kwa sababu hutumia muda mwingi sana kutoka eneo moja hadi lingine kufuata huduma fulani kutokana na miundombinu mibovu na kukosekana kwa mawasiliano na pia wananchi hutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya.
“Katika Tarafa ya Sale pamoja na maeneo mengine imekua ni vigumu sana kutoa msaada wa haraka wakati wa dharura kwa sababu hakuna hata mtandao mmoja unaopatikana na kuna baadhi ya makampuni yamejenga minara ya Simu kwa kipindi kirefu bila kuleta huduma hiyo sasa sielewi hiyo minara ilijengwa kwa ajili ya kazi gani”
Akijibu hoja hizo zilizowasilishwa kwake Mkuu wa Mkoa Mhe. Gambo amesema atawasiliana na Kampuni ya Halotel ambao wana wajibu wa kuleta huduma za mawasiliano vijijini ili waweze kuleta huduma hiyo haraka katika maeneo haya kwa kuwa wote hawa ni wananchi wa Mkoa wa Arusha na wanahitaji huduma hii ya mawasiliano kama walivyo wananchi wote wa Mkoa Arusha. Aliendelea kufafanua kwamba Kampuni hii ilianzishwa ili kutatua changamoto katika maeneo ya pembezoni kama haya ya Ngarasero.
Aidha Gambo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kwamba Kata hii inajengewa Kituo cha Afya katika mwaka wa Fedha 2016/2017 kwa sababu uhitaji ni mkubwa na wananchi hawa wanapata shida kwa sababu ya umbali uliopo wa huduma hizi na changamoto ya miundombinu ya barabara inayowakabili hivyo huchukua muda mrefu kuzifikia huduma hizo na pengine kusababisha madhara zaidi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ametembelea Kata ya Ngaresero, Penyinyi, Digodigo, Samunge, Oldonyosambu na Loliondo na katika maeneo yote hayo amezungumza na wananchi na kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili.
No comments:
Post a Comment