Wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za serikali na makampuni binafsi walijitokeza kwa wingi mwishoni mwa wiki kushiriki matembezi ya hisani ya kuchangia matibabu ya saratani katika taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa kampuni ambayo wafanyakazi wengi walijitoa muda wao kushiriki katika tukio hilo la hisani ni kampuni ya TBL Group
Baadhi ya washiriki wa matembezi hayo walieleza kuwa wameguswa na changamoto zilizopo katika kukabiliana na ongezeko kubwa la wagonjwa wa Saratani nchini na kuahidi kuwa watazidi kujitoa kusaidia wahanga wa ugonjwa huu na kufikisha elimu kwenye jamii jinsi ya kuutambua na kuwahi kupata matibabu zinapojitokeza dalili za ugonjwa huu ambao unazidi kusababisha vifo vya wananchi wengi
Washiriki wa matembezi ya kuchangia wahanga wa Saratani ya matiti wakijiandaa kuanza matembezi katika viwanda vya taasisi ya Ocean Road

Bendi ya polisi ikiongoza matembezi
Shamrashamra mbalimbali za uhamasishaji zilikuwepo
Zoezi la kutembea na mazoezi likiendelea
No comments:
Post a Comment