WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea maeneo yaliyopendekezwa kujengwa mji wa Serikali na kujiridhisha kuwa yanatosha kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu.
Katika ziara hiyo aliyoifanya leo mchana (Jumatatu, Oktoba 3, 2016) Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ukubwa wa maeneo hayo ambayo pia yanatosha kujenga miundombinu inayohitajika.
Katika ziara hiyo Waziri mkuu ameridhishwa na maeneo yaliyotengwa na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu(CDA) yanayofaa kuwekeza kwa ujenzi wa miundombinu ya biashara kama masoko na hoteli na viwanda na tumejirishisha kuwepo kwa ardhi ya kutosha.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amekaribisha wawekezaji wa miradi mbalimbaliya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za watumishi ambao watajenga nyumba za makazi na kuziuza kwa watumishi wa umma na wananchi.
Aidha amebainisha kuwa muwekezaji atakayekuwa tayari awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye ndiye anayeratibu shughuli hiyo huku akikaribisha wawekezaji wa ujenzi wa hoteli za kitalii na kawaida kwa kuwa wanatarajia kupata wageni wengi.
“Tumekaribisha pia wawekezaji wa ujenzi wa viwanda tumeiona ardhi inatosha na uzalishaji ni mkubwa Kanda ya kati kwa mkoa wa Dodoma wenyewe, Manyara, Singida na mikoa ya jirani ya Iringa na Morogoro inaweza kunufaika na fursa hizo,” amesema.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), Mhandisi Paskasi Muragili alisema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo ambayo Waziri Mkuu alimeyatembelea ni Chigongwe lenye hekta 11,297, Kikombo hekta 13,275 na Nyankali hekta 2,370
No comments:
Post a Comment