• Breaking News

    Wednesday, 10 August 2016

    Serena Williams achapwa katika michuano ya Olimpiki

    Serena Williams achapwa katika michuano ya Olimpiki


    Bingwa huyo wa dunia alionekana na kufanya makosa mara tano mfululizo
    Image captionBingwa huyo wa dunia alionekana na kufanya makosa mara tano mfululizo
    Bingwa mtetezi Serena williams ametupwa nje ya mashindano ya michezo ya Olimpiki baada ya kushindwa na mchezaji wa Ukraine Elina Sitoniva katika hatua ya tatu ya tennis ya mashindano ya wanawake.
    Williams ameshindwa kwa seti 6-4-6-3 na Sitovia ambae anashika nafasi ya 20 duniani.
    Bingwa huyo wa dunia alionekana na kufanya makosa mara tano mfululizo katika raundi ya saba kipindi cha pili.
    "haikua kama nilivyokua nataka iwe lakini angalau nimweza kufuzu kuja Rio, hilo lilikua kati ya malengo yangu" amesema William.
    Serena Williams
    Image captionSerena Williams Z4newsblog.blogsport.com
    " Mchezaji mzuri leo ameshinda leo lakini najua kuwa wakati mwingine utakua mchezo mzuri sana na nasubiri wakati huo"
    William na mdogo wake Venus wametolewa katika mashindano ya wawili ya wanawake siku ya jumapili na raia wa jamhuri ya watu wa Cze, Lucie Safarova na Barbora Strycova.

    No comments:

    Post a Comment