• Breaking News

    Wednesday, 10 August 2016

    Hillary Clinton afunguliwa kesi kwa mauaji ya Libya 2012

    Hillary Clinton afunguliwa kesi kwa mauaji ya Libya 2012



    Mapema mwaka huu Clinton alisafishwa kutohusika na mauaji hayoImage copyrighttembelea you tube andika z4tv channell utatupa live
    Image captionMapema mwaka huu Clinton aliondolewa lawama kuhusiana na mauaji hayo

    Wazazi wa wamarekani wawili waliouliwa miaka minne iliyopita nchini Libya wanamshutumu mgombea Urais kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton, kwa kuchangia kutokea kwa mauaji hayo.
    Clinton waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani kipindi ubalozi wa Marekani nchini Libya uliposhambuliwa.
    Patricia Smith na Charles Woods, ambao ni wazazi wa Sean Smith na Tyrone Wood wamesema kuwa matumizi ya barua pepe binafsi zilichangia mauaji ya watoto wao.

    Patricia Smith, mama wa Sean Smith amemlaumu Clinton kwa kifo cha mtoto wakeImage copyright
    Image captionPatricia Smith, mama wa Sean Smith amemlaumu Clinton kwa kifo cha mtoto wake

    Msemaji wa kampeni za Hilary Clinton amepinga tuhuma hizo. Ingawa kamati ya Chama cha Republican inaweka wazi mabaya aliyoyatenda Hilary, jambo linalo tia doa kampeni zake za Urais.
    Uvamizi wa majeshi ya kiislam katika ubalozi wa Marekani uliwauwa raia wanne wa nchi hiyo akiwemo Balozi Chris Stevens.

    No comments:

    Post a Comment