• Breaking News

    Wednesday, 10 August 2016

    Ranieri aongeza mkataba Leicester City

    Ranieri aongeza mkataba Leicester City


    Claudio Ranieri
    Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Leicester City wamemuongezea mkataba wa miaka minne kocha wao Claudio Ranieri.
    Mkataba huo mpya utamuweka kocha huyo raia wa Italia, mwenye umri wa miaka 64, kwa mabingwa hao mpaka mwezi Juni, mwaka 2020.
    Ranieri anaungana na wachezaji Kasper Schmeichel, Wes Morgan na Jamie Vardy waliongeza mikataba ya muda mrefu katika klabu hiyo.
    Makamu mwenyekiti wa timu hiyo Aiyawatt Srivaddhanaprabha, amesema kocha huyo yuko katika mpango wa muda mrefu wa timu hiyo kwa kuwa na ujuzi mkubwa na uzoefu.
    Katika msimu wake wa kwanza kocha huyo aliwapa ubingwa timu hiyo Ranieri amewahi kuvifundisha vilabu vikubwa kama Chelsea, Juventus, Inter Milan na AS Roma.

    No comments:

    Post a Comment