Mtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine sita kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa kwa kutumia kisu katika mji mkuu wa Uingereza, London.
Polisi ya Uingereza ambayo imemtia nguvuni mtu aliyetekeza shambulizi hilo katika Medani ya Russell, imesema kuwa kuna uwezekano shambulizi hilo likawa la kigaidi.
Msaidizi wa kamanda wa polisi ya London, Mark Rowley, anasema ishara za awali zinaonesha kuwa matatizo ya kakili ni sababu kuu ya shambulizi hilo lakini amesisitiza kuwa, ni vigumu kukanusha uwezekano kwamba limefanyika kwa sababu za kigaidi.
Ulinzi waimarishwa London |
Shambulizi hilo la kutumia kisu limefanyika siku moja baada ya vyombo vya usalama vya Uingereza kuimarisha usalama katika mitaa ya jiji la London kwa kuzidisha idadi ya polisi wenye silaha baada ya kuongezeka vitendo na hujuma za kigaidi barani Ulaya.
Wanachama wa kundi la Dola ya Kiislam (Daesh) wamezidisha mshambulizi yao katika nchi za Ulaya katika siku za hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment