• Breaking News

    Tuesday, 9 August 2016

    AMTEUA MKEWE KUWA MGOMBEA MWENZA WAKE


    Rais wa Nicaragua, Daniel Ortega, amemteua mkewe, Rosario Murillo kuwa mmgombea wake mwenza wakati akigombea kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu. Kwa sasa Rosario ni msemaji mkuu wa serikali ya mumewe na anaonekana kama mbiya wa madaraka ya mumewe.


    Rosario ambaye ni mama wa watoto saba ni maarufu sana kwa kuvaa mavazi ghali na vidani vya thamani ya juu. Hapo jana Ortega na mkewe walikubali rasmi uteuzi wa chama chao uliowapa nafasi hiyo. Aliingia madarakani mwaka 2007.

    No comments:

    Post a Comment