Manchester United imekamilisha usajili wa Paul Pogba uliovunja rekodi kwa kitita cha £100 milioni.
Kiungo huyo ghali zaidi duniani kwa sasa amewasili akitokea Juventus, kuungana na klabu ambayo aliiacha mwaka 2012.
Pogba, 23, anatarajiwa kuvaa jezi namba 6 na amesaini kitita cha £290,000 kwa wiki, mkataba wa miaka 5 chini ya Jose Mourinho. Pia ana uhuru wa kuongeza mwaka mwingine zaidi.
Paul Pogba katika jezi ya Manchester United kwa mara ya kwanza baada ya kukamilisha uhamisho wake. |
Nyota huyo wa Ufaransa ni maarufu kwa mitindo ya nywele zake na mara hii ameweka nembo ya klabu ya United katika mtindo wa nywele zake. |
No comments:
Post a Comment