Kiungo wa Tusker FC,Brian Osumba ameapa kwamba watatoa ushindani wa hadi dakika ya mwisho kwa Gor Mahia na hatimaye kunyakua taji la KPL msimu huu.
Osumba anaamini fomu waliyonayo kwa sasa kwenye kikosi hicho,ni jambo ambalo linazidi kuimarisha makali yao.Mabingwa hao wa mara 10 wa KPL wameandikisha msururu wa matokea mazuri katika mechi tatu zilizopita na kujiweka kwenye nafasi ya nne.
Akieleza kwamba hiyo ni sababu inayowafanya wajiamini ndani ya kikosi hicho,Osumba alisema kwamba wanalenga kuwafunga Mathare United kesho huko Ruaraka na kupunguza pengo baina yao na Gor Mahia hadi alama sita.
’’Kwa sasa hatuna shinikizo lolote kwa kuwa tumefaulu kuyaweka hai matumaini ya mashabiki wetu.Ni afueni kubwa kuona kila mmoja ameyarejelea makali yake licha ya kuanza msimu kwa matao ya chini.Kikubwa tunachohitaji ni kujivunia alama nyingi zaidi na kuwaongezea K’Ogalo presha.Hapana shaka kwamba watavaliwa na wasiwasi na kupoteza alama muhimu’’alisema Osumba.
Akiyaunga mkono mawazo ya nyota wake,kocha Francis Kimanzi alisema kwamba kikosi chochote miongoni mwa tano bora kufikia sasa kina uwezo mkubwa wa kulinyakua taji la msimu huu.
‘’Ni furaha kukishuhudia kikosi kikiimarika baada ya kila mechi,Nina wingi wa matumaini kwamba mambo yatazidi kuwa shwari kwa upande wetu kadri ushindani unapozidi kushika kasi.Timu zote zinaongozwa na azma ya kuibuka na ushindi hasa ikizingatiwa tofauti ndogo ya alama ambazo zinatutenganisha na timu saba zilizopo nyuma yetu.
No comments:
Post a Comment