• Breaking News

    Wednesday, 13 May 2015

    TAIFA STARS WAWASILI AFRIKA YA KUSINI



    Msafara wa Taifa Stars ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, umewasili salama katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa OR Tambo usiku huu jijini Johanesburg ,nchini Afrika ya Kusini na kupokelewa na watanzania wanaoishi nchini humo.
    Taifa Stars imekwenda nchini Afrika Ya Kusini ili kushiriki kwenye michuano ya COSAFA ,inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini.Ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.
    Taifa Stars iliondoka jijini Dar es salaam leo majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri wa shirika la ndege la Fasjet.

    No comments:

    Post a Comment