Na Musa Mwakisu,Dar Es Salaam.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Azam Fc,zimeijulisha mwakisusports mkufunzi huyo wa zamani wa klabu hiyo,raia wa Uingereza Stewart John Hall mwenye mahaba ya kupindukia na soka la Tanzania amerejea kwenye klabu hiyo baada ya kufanya mazungumzo na wamiliki wa klabu hiyo,na ambapo kulipitishwa maamuzi ya kufanyika upigwaji wa kura ambao ulihusisha viongozi na wachezaji wote wa Azam,na hatimaye wingi wa kura ulionyesha kuwa Stewart John Hall amekuwa kinara kwa kupata kura nyingi zilizohitaji apewe nafasi ya kurejea tena kwenye timu hiyo.
Kura hizo zilipigwa ili kutazama imani ya wachezaji juu ya mkufunzi huyo wa zamani wa klabu hiyo,ni hali iliyotokana baada ya hapo zamani kuwepo kwa maneno mengi ya uzushi kuwa ni mtu ambaye hakubaliki na wachezaji ndani ya klabu hiyo,hali ambayo ilichangia kwa timu hiyo kuachana naye mwishoni mwa msimu wa 2013/2014.
Stewart Hall anachukua kijiti kilichomchoropoka Joseph Marius Omog,ambaye alifurushwa kwenye kibarua jicho mwezi wa pili mwaka huu,baada ya Azam kutolewa kwenye mzunguko wa kwanza wa michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika na El Merreikh ya Sudan.
Kwa sasa George ‘Best’ Nsimbe ndiye kocha mkuu wa muda na msaidizi wake ni Dennis Kitambi,ambao Azam FC wameshindwa kutetea ubingwa walioupata msimu uliopita chini ya mkufunzi Joseph Marius Omog.
No comments:
Post a Comment