• Breaking News

    Thursday, 14 May 2015

    STARS YAWASILI RUSTENBURG

     Na Baraka Kizuguto,Rustenburg,Afrika Ya Kusini.

    Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili leo mchana majira ya saa 6 kamili katika jiji la Rustenburg na kufikia katika hoteli ya Hunters Rest - Protea iliyoypo pembeni kidogo ya  jiji.

    Taifa Stars ambayo iliondoka jana joni jijini Dar es salaam jijini Dar es salaam na kufika OR Tambo saa 5 usiku, ilipata mapokezi mazuri kutoka kwa waandaji wa michuano ya COSAFA pamoja na watanzania wanaoishi jijini humo, ililala katika hoteli ya Southern Sun.

    Safari ya kutoka Johannesburg kuelekea Rustenburg ilichukua takribani masaa mawili na msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ephaphra Swai.

    Wachezaji waliopo na timu Rutsenburg ni Deogratius Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Salim Mbonde, Aggrey Moriss, Joram Mgeveke, Said Juma, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto, Ibhrami Ajib, Juma Luizio, John Bocco, Mrisho Ngasa na Saimon Msuva.

    Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kufanya mazoezi leo  
    jioni katika uwanja wa Rustenburg Impala Bowling Club majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Kusini sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.

    No comments:

    Post a Comment