• Breaking News

    Tuesday, 12 May 2015

    TAIFA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO

    Na Baraka Kizuguto,Dar Es Salaam.


    Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.

    Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng  jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.

    Taifa Stars itaondoka jijini Dar es salaam kesho majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri wa shirika la ndege la Fasjet na kufika jijini Johanesburg saa 5 usiku.

    Mara baada ya kupimwa afya jana na madaktari wachezaji Aishi Manula, Isihaka Hassan, Haroun Chanongo, Kelvin Friday na nahodha Nadir Haroub wamekutwa na majeruhi ambayo yamepelekea kutokuwepo katika kikosi kitakachosafiri kesho, watabakia nchini wakiendelea kufanya mazwoezi chini ya ungalizi mpaka timu itakaporejea kutoka Afrika Kusini na kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON, huku Amri kiemba akipewa ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

    Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, timu inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Sun City iliyopo pembeni kidogo ya jiji la Rusterburg.

    No comments:

    Post a Comment