• Breaking News

    Friday, 8 May 2015

    RAIS TFF ATUMA SALAMU ZA POLE KWA WAHANGA WA MAFURIKO

    Na Baraka Kizuguto,Dar Es Salaam.
    Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal  M
    alinzi ametuma salaam za pole kwa wakazi wa Dar es salaam na hasa wale walioathirika na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam kwa siku ya tatu mfululizo sasa.

    Katika salam zake kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Mecky Sadik, Malinzi amesema familia zimepoteza makazi, miundombinu ya usafiri na michezo imeharibika na hata kuwa katika hali ya kutotumika, wanawake watoto, familia, shughuli za kiuchumi na kimichezo zimeathirika na mvua hizi.

    TFF inaunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Serikali na wadau wote wanaoshugulika  kupunguza makali ya janga hili.

    No comments:

    Post a Comment