• Breaking News

    Thursday, 14 May 2015

    Garry Monk anastahili zaidi heshima England

    Na Musa Mwakisu
    Ni mtanashati kama walivyo wacheza ngoma za kinyasa,akivaa suti yake ni vigumu vioo vya wapiga picha kushindwa kuelekea kwake,ijapokuwa ni mwalimu anayefundisha mchezo wa soka wenye presha nyingi lakini hajawai kupatwa na ajali ya kupotezwa kwa utanashati wake akiwa kwenye majukumu yake.


    Garry Monk ni mzaliwa wa Bedford, England amekuwa ni mwalimu kijana aliyefanya vema msimu huu kwenye ligi ya England akiwa na Swansea City,ameweza kujipatia alama 56 ya michezo 36 ya timu yake ni timu iliyotumia bajeti ndogo msimu huu wengi walimuweka kwenye fungu la mkufunzi atakayepaka mkorogo taaluma yake hadi kupelekea Swansea kudidimia.Twakwimu chanya za msimu huu za kikosi cha Swansea zmebadirisha kila kitu kwenye maisha ya soka ya Garry Monk.


    Kwa mwalimu wa aina yake aliyedharauliwa mwanzoni mwa msimu,lakini kwa sasa ameweza kufanya kile kinyume ambacho watu waliotarajiwa ameweza kuchukua alama 12 kwa mkupuo msimu huu kwa maadui wa soka la England(Man United na Arsenal)timu zinazoundwa kwa bajeti kubwa na zilizosheheni wachezaji wengi waliostawi zaidi na soka la kimataifa.


    Dunia ya wafuatiliaji wa soka la England,imekuwa likisita kumpa heshima stahiki mkufunzi huyu tofauti na sifa wanazopata wakufunzi wengi wenye umri wa kutosha na waliokuwa kwenye timu zenye kuzungumzwa mno.Garry Monk ni mkufunzi ambaye anaweza kukupa radha zote za soka,kuna baadhi ya mechi anaweza kupaki bus kwa aslimia 75 na mechi nyingine akaamuwa kucheza soka la kushambulia kwa asilimia 75.


    Ni vema kumtazama mkufunzi huyu kwa jicho jingine kwa umri wake anaweza kuwa msaada mkubwa kwenye soka la England ambalo limetawaliwa mno na walimu wa kigeni kwenye ligi kuu ya England na kumpa heshima stahiki kutokana na kazi aliyoifanya kwenye kikosi cha Swansea msimu huu.

    No comments:

    Post a Comment