Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkingaakifungua Mkutano wa Jukwaa la kuwatia moyo wanawake katika kufanya utafiti na kuwa wabunifu ili kutumia fursa zilizopo nchini lengo likiwa ni kuwakutanisha wanawake wanasayansi waliofanikiwa katika sekta hiyo na wasichana au wanawake wengine kwa lengo la kuwapa hamasa kupitia changamoto walizokumbana nazina namna walivyoweza kuhimili na kufanikiwa katika kufikia ndoto zao
Wanawake wanapaswa kujiamini na kuishi maisha ya ndoto zao mbali na changamoto lukuki wanazokutana nazo katika Tafiti zao ama shughuli zao za kila siku kwani wamebarikiwa vipaji tofauti na kwa wale wasichana wanaoogopa masomo ya sayansi kwa kuwa wameambiwa ni magumu wanatakiwa kuziba masikio na kusoma kwa bidii katika masomo ya sayansi.
Jambo ambalo litawafanya kufanikiwa katika ngazi ya familia zao mpaka katika taifa katika nyanja za Udaktari, Utafiti.Mitindo na Uchoraji, ambapo wanafunzi wa kike kutoka sekondari za Benjamin Mkapa walieleza ndoto zao kwa siku za usoni kuwa ni wanawake watakaoleta mabadiliko chanya katika jamii hasa katika masuala ya Sayansi Mkutano huo unafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam .
Dk. Mwele Malecela Mkurugenzi Mkuu wa National Institute for Medical Research (NIMR) akizungumza na wanawake wanasayansi na watafiti wakati wa mkutano huo uliofanyika unaofanyika kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam.
Dk Eliza Shayo mtafiti mwandamizi akichangia mada katika mkutano huo.
Baadhi ya wanawake watafiti wakiwa katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment