• Breaking News

    Thursday, 6 October 2016

    SERIKALI YAWATAKA WANANCHI WAUNDOKE MAENEO YA MASHULE

    Waziri wa Tamisemi GEORGE SIMBA CHAWENE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO ,JIJINI DAR ES SALAAM.

    SERIKALI imewataka wananchi walivamia maeneo ya shule kuondoka mara moja kwani kuendelea kukaa katika maeneo hayo nikinyume cha utaratibu wa mipango miji .

    Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene amesema serikali imetoa marufuku kwa baadhi yawananchi wanaojenga vyumba vya biashara sambamba na maeneo yanayozunguka shule kwani kitendo hicho kinasababisha mwingiliano wa shughuli zinazotakiwa kufanyika katika maeneo hayo .

    ''Maendelezo yoyote yaliyofanywa kama biashara na yanayotarajiwa kufanywa kama biashara katika maeneo yashule hayarusiwi ,aidha shule zote zilizopo mjini zihakikishe zinajenga uzio unaozunguka maeneo hayo ''Alisema WAZIRI wa Tamisemi George Simbachawene .

    Waziri wa Tamisemi Simbachawene alisema kuwa wananchi waliovamia maeneo yataasisi hizo waondoke wao wenyewe watakao kiuka agizo hilo nguvu zakisheria zitatumika .
    Alisema kufuatia agizo hilo amewataka wakuu wamikoa nawakuu wa wilaya kuweza kusimamia zoezi hilo kikamilifu kwenye mamlaka za serikali za mitaa zilizopo katika maeneo yao .
    ''Nawataka watendaji wa serikali kulisimamia zoezi hili la kuwahamisha waliovamia maeneo yashule kuondoka maramoja kabla miezi mitatu ''Aliongeza Simba chawene .

    No comments:

    Post a Comment