Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Shabani Pazi akizungumza wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) kufunga Semina ya uandaaji wa mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mitandao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza wakati akifunga warsha ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola (hawapo pichani) kuhusu uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao nchini.
Afisa Mwandamizi wa ufundi na ushauri wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Bw. Fargani Tambeayuk akitoa shukurani kwa wadau na Wizara baada ya kumalizika kwa warsha ya uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mitandao
Wadau wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati akifunga Semina ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola Jijini Dsm.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment