Yaya Toure ameachwa katika kikosi cha Manchester City kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Ikumbukwe kuwa Toure alishawahi kuwa chini ya Guardiola wakati yupo Barcelona na kupata wakati mgumu kabla ya kuamua kuondoka na kuhamia Manchester City.
Tayari Guardiola ameshawatoa kwa mkopo Joe Hart, Samir Nasri, Wilfried Bony na Eliaquim Mangala na kuleta mtikisiko kwenye klabu hiyo yenye maskani yake kwenye dimba la Etihad.
Toure amebakia klabuni hapo baada ya dirisha la usajili kufungwa juzi usiku.
Toure (33) alicheza dakika zote tisini kwenye mchezo wa raundi ya pili wa kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest, lakini jina lake halijajumuishwa kwenye kikosi hicho kinachoundwa na wachezaji 21.
Wachezaji wapya kama Claudio Bravo, John Stones, Ilkay Gundogan, Leroy Sane na Nolito wote wamejumuishwa kwenye kikosi hicho ambacho kitavaana na Barcelona, Borussia Monchengladbach na Celtic kwenye Kundi C
No comments:
Post a Comment