Ukimya wa Real Madrid katika soko la usajili umewafanya mabingwa hao wa ulaya kuweka rekodi ya kutumia Fedha kidogo zaidi kwenye usajili katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, huku wakiwa na hatari ya kufungiwa kwa vipindi viwili vya usajili.
Real wametumia kiasi cha Euro million 30 walizowalipa Juventus kumrudisha Alvaro Morata kikosini kutokea Turin.
Hivyo tangu walipomnunua David Beckham mwaka 2003, mwaka huu ndio wametumia kiasi kidogo zaidi katika kuimarisha kikosi chao. Mwaka huo, Raisi wa Madrid Florentino Pérez alitumia 25 million euros kumsajili nahodha hiyo wa zamani wa England.
2009: Msimu wa gharama zaidi
Wakati mwaka 2003 walitumia kiasi kidogo zaidi, msimu wa 2009/2010 ndio msimu ambao Madrid walitumia fedha nyingi zaidi, walitumia jumla ya 259 million kufanya usajili. Huu ndio msimu ambao Perez alirejea madarakani na kuwasajili Cristiano Ronaldo (96 million), Kaká (65), Karim Benzema (35) na Xabi Alonso (30)
No comments:
Post a Comment