• Breaking News

    Monday, 29 August 2016

    WANAFUNZI WA CHUO CHA DIPLOMASIA WAMNUNULIA MWENZAO VIFAA VYA

    1

    Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia Dk Bernald Achiula akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo wakati akishukuru wanafunzi wa chuo hicho kwa michango yao waliyochanga ili kumsaidia mwanafuzni mwenzao Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ana matatizo ya kusikia, wanafunzi hao wamechanga Fedha na kumnunulia mwenzao Vifaa vya kumsaidia kusikia vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano,  Kulia ni Mwanafuzni  Shinuna Salum Nyamkokwa  ambaye ameelezewa kuwa ana uwezo mkubwa katika masomo yake darasani pamoja na kutokuwa na uwezo wa kusikia,  na Katikati ni Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.
    2
    Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia akielezea kwa waandishi wa habari kuwa kitu kilichowafanya  wanafunzi  wa chuo hicho kumchangia mwanafunzi mwenzao Shinuna Salum Kulia  ni kutokana na uwezo wake katika masomo pamoja kuwa tatizo la usikivu linalomkabili
    3
    Mwanafuzni huyo Shinuna Salum Nyamkokwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea kuhusu msaada wa vifaa hivyo ambapo amesema awali kichwa kilikuwa kinamuuma sana lakini kwa sasa hakiumi tena.
    4

    Gordian Kilave Mkuu wa Idara ya Lugha Chuo cha Diplomasia akielezea matatizo yaliyokuwa yakimkuba na kumsumbua mwanafunzi Shinuna Salum kabla ya kupatiwa vifaa hivyo ambavyo ninamsaidia kusikia kwa sasa. 

    No comments:

    Post a Comment