• Breaking News

    Monday, 29 August 2016

    NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo, amesema.

    Image result for naibu waziri jafoNAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo, amesema Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, ina wanafunzi hewa 4445 ambao wanasoma katika shule za sekondari za serikali kinyume na utaratibu.
    Jaffo aliyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri za Msalala na Mji, juzi, katika ziara ya kushitukiza, ambapo aliwaasa kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata sheria na taratibu za kuwahudumia wananchi.
    Alisema kuwepo kwa idadi hiyo kubwa ya wanafunzi hewa katika shule za sekondari kunatokana na maofisa elimu kutokujua takwimu za wanafunzi na kuongeza kuwa, muda mwingi wamekuwa wakikaa ofisini bila ya kutembelea maeneo ya kazi.
    Naibu Waziri huyo alisema, takwimu za utengenezaji wa madawati, zimekuwa kinyume na ilivyotarajiwa, hali ambayo imesababisha kuchelewa kumalizika kama iliovyokuwa imepangwa na Rais John Magufuli.
    Pamoja na mambo mengine, Naibu Waziri huyo aliwaonya watumishi hao kutotumia fedha vibaya zitakazotolewa na wizara hiyo, kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya barabara katika halmashauri ya mji wa Kahama.
    Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Halmashauri ya Mji wa Kahama, ina changamoto nyingi zikiwamo za miundombinu ya barabara, kuzidiwa kwa wagonjwa wanaotoka katika wilaya 16 katika hospitali ya halmashauri ya mji pamoja na upungufu wa watumishi.
    Alisema Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama, imezidiwa na wagonjwa ambao wanatoka katika sehemu mbalimbali zilizopo jirani, hali ambayo watumishi wake wanapata wakati mgumu katika kutoa huduma na wakati mwingine kushindwa kutoa huduma kwa wakati

    No comments:

    Post a Comment