• Breaking News

    Wednesday, 10 August 2016

    Putin akubali kurejesha ubalozi na Uturuki


    Rais wa Russia, Vladimir Putin amekubali kufanya juhudi za kurejesha tena kwa kikamilifu uhusiano wa kibalozi na Uturuki, lakini akasema kuwa kuujenga tena uhusiano wa kibiashara kutachukua muda mrefu.
    Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Uturuki Tayyip Erdogan mjini Petersburg jana Jumanne, Putni alisema kwamba kuna kazi nyingi iliyo mbele ya kuufufua ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili. Alisema kazi hiyo imeanza lakini itachukua muda mrefu.
    Erdogan alisema mataifa hayo mawili yatarejesha ushirikiano wa kila mwaka uliolenga bishara ya kiasi cha dola bilioni mia moja na kuongeza kasi mazungumzo juu ya kuanza tena kwa safari za ndege.

    No comments:

    Post a Comment