Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha, Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (DPC).
Taarifa ya Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo imeeleza kuwa Msigwa amethibitishwa kuanzia leo Agosti 31, 2016 kushika wadhifa huo.
Kabla ya uthibitisho huo, Gerson Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015
No comments:
Post a Comment