• Breaking News

    Wednesday, 10 August 2016

    Donald Trump alaumu wanahabari kufuatia utata kuhusu bunduki

    Donald Trump amewalaumu waandishi wa habari baada yake kushutumiwa kwa matamshi yake ambapo alidaiwa kuwahimiza wafuasi wake wamuue mpinzani wake Hillary Clinton wa chama cha Democratic. Alikuwa amewaambia wafuasi wake kuwa wanaweza kumzuia hasimu wake Bi Clinton kwa kutekeleza haki zao za silaha. Alisema Bi Clinton anaweza kupeleka haki zake huria za kisheria mbele ya Mahakama ya Juu kama atashinda urais mwezi Novemba, na kufuta haki ya raia kumiliki silaha. Akihutubia mkutano wa kisiasa katika jimbo la North Carolina, Bw Trump alidokeza kuwa haki za umiliki wa silaha zinaweza kusaidia kumzuia Bi Clinton kuchukua mamlaka. Kauli yake hiyo imezua hasira kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimshutumu kwa kuchochea ghasia. Lakini muda mfupi baadaye alijitetea na kusema kuwa alikuwa tu anawataka wanaounga mkono haki za umiliki wa silaha kupiga kura kwa wingi. Baadaye alisema wanahabari wa shirika la habari la Fox News walipinda matamshi yake na kuyafanya yaonekane kana kwamba alikuwa anawahimiza wafuasi wake wenye silaha wazitumie kumuangamiza Bi Clinton. Hii si mara ya kwanza kwa Bw Trump kulazimika kukosoa kauli zake

    No comments:

    Post a Comment