Klabu ya Yanga SC imeendelea na harakati zake za kuimarisha timu hiyo baada ya leo hii kumsajili mshambuliaji wa Mgambo JKT ya Tanga. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Yanga Sc,DK Jonas Tiboroha amesema Malimi Busungu amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea timu hiyo msimu ujao.
Mchezaji huyo inasemekana alikuwa akiwania pia na watani wao halisi katika soka la bongo timu ya Simba,ambapo ilipelekea thamani ya mchezaji huyo kupanda zaidi kwenye kugombania sahihi yake.lakini katika mbio hizo kama inavyoonekana pichani ni rasmi Yanga wamekuwa vinara kwa kuweza kupata huduma ya mshambuliaji huyo ambaye ameitwa hivi karibuni kwenye kikosi cha timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment