Na Mwandishi wetu.
Kenya ilirushwa kutoka nafasi ya tatu mwaka jana hadi ya saba katika Mbio za Dunia za Kupokezana Vijiti(Relays),ambazo zilikamilika nchini Bahamas mapema jana.
Matokeo haya ni duni haswa baada ya Kenya kumaliza nyuma ya miamba wa mbio fupi Marekani na Jamaica miezi 12 iliyopita.Wakati huo,Kenya ilichukua mataji ya wanaume na wanawake wa mita 4x 1500 na kushinda dhahabu mita 4x800 wanaume na fedha mita 4x800 wanawake.Katika mashindano ambayo yalikamilika jana,Marekani,Jamaika,Poland,Australia,Ujerumani na Ufaransa zilinyakua nafasi ya sita za kwanza katika usanjari huo.
Kenya ambayo ilishiriki vitengo vya wanaume vya mita 4x200,4x400,4x800 na ‘’medley’’na kinadada 4x800 na ‘’medley’’ilipata nishani mbili tu.Medali za Kenya zilipatikana katika kitengo chipya cha ‘’medley’’kinachojumuisha mita 4000 ambapo kuna mkimbiza upepo wa mita 1200,400,800 na 1600.
Kitengo hiki kilichukua mahala cha kile cha 4x1500.Kenya haikuwa na bahati baada ya kuondolewa mashindanoni katika mita 4x200 na 4x800(Wanaume)kwa kuvunja sheria za kupokezana vijiti na kumaliza katika nafasi ya 12 katika 4x400(Wanaume)
Picha hii na maktaba
Marekani ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia baada ya kutawala vitengo saba katika 10 jijini
Nassau.Walikuwa na miwango duni kwenye katika mita 4x200,lakini hayakuathiri msimamo wao kwenye jedwali baada ya kuzoa alama 63,tatu zaidi ya zile walizopata mwaka jana.
Ushindi wao wa medali saba ulikuwa pia ni rekodi ya dunia katika’’medley’’wanaume na kinadada na rekodi za mashindano hayo katika mita 4x800 wanaume na akinadada pamoja na wanaume 4x100 na wanawake 4x400.
Jamaika pia ilisalia nambari mbili baada ya kupata alama 46.Timu ya Jamaica,ambayo ilikuwa na mshindi wa rekodi ya dunia mita 100na 200,ilishinda wanaume 4x200 na wanawake 4x100m.
Poland walipanda kutoka nambari tisa mwaka 2014 hadi tatu mwaka huu baada ya kuzoa alama 34.Walipata nishani ya fedha katika mita 4x800 wanaume na wanawake,miongoni mwa medali zingine.Australia pia waliimarika kwenye msimamo wa dunia kutoka nafasi ya tano hadi ya nne.
No comments:
Post a Comment