Na Musa Mwakisu
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, Benni McCathy ameripotiwa kukumbwa na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha katika eneo la Melrose Arch mchana wa leo. Kwa mujibu wa tovuti ya Kickoff.com, McCarthy alitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa OR Tambo saa 5 asubuhi kabla ya kwenda moja kwa moja kwenye saluni yake anayoipenda sana katika eneo hilo la Melrose Arch mjini Johannesburg.
Chanzo kilicho karibu na mchezaji huyo aliyewahi kuwika na klabu ya Orlando Pirates, kimesema kuwa wahalifu watatu wenye silaha waliingia katika saluni hiyo na kuchukua vitu vyake vya thamani. Tukio hilo lilitokea takribani saa 7 mchana, huku washukiwa hao wakisadika kuondoka katika eneo la tukio ndani ya gari nyeusi aina ya BMW. “Watu watatu wenye silaha waliingia ndani ya saluni, mmoja akasimama mlango kwa ajili ya ulinzi, mwingine akawaweka chini ya ulinzi wateja waliokuwa humo huku wa tatu akienda moja kwa moja kwa Benni na kuchukua saa, hereni na pete yake ya ndoa,” kilisema chanzo hicho. “Watu hao hawakuwabughudhi wateja wengine na walielekea moja kwa moja kwa Benni kana kwamba walikuwa wakifuatilia nyendo zake. "Walipochukua walichotaka, waliondoka katika gari nyeusi aina ya BMW, ya mwaka 2007, yenye vioo vyeusi.
“Inaelezwa kuwa Benni bado ana mshituko kutokana na tukio hilo, lakini yuko salama na hakupata madhara yoyote,” kiliongeza chanzo hicho
Mshindi huyo wa mara moja wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, UEFA, ambaye kwa sasa anasaka kibali cha ukocha cha daraja A kutoka UEFA, ni miongoni mwa watu maarufu wa Afrika Kusini waliokumbwa na visa vya kutisha vya unyang’anyi katika miezi ya hivi karibuni. Mwaka uliopita, Senzo Meyiwa alipigwa risasi na kuuawa wakati kile kinachodhaniwa kuwa ni wizi wa kutumia silaha uliotokea nyumbani kwa mpenzi wake, Kelly Khumalo, katika eneo la Vosloorus mashariki mwa mji wa Johannesburg.
Kiungo wa Bidvest Wits na Bafana Bafana, Sibusiso Vilakazi na kocha Shakes Mashaba ni miongoni mwa waathirika wa visa vya ujambazi katika miezi ya hivi karibuni.

No comments:
Post a Comment