• Breaking News

    Sunday, 19 April 2015

    TFF YAUNGA MKONO KAULI YA COSAFA

    Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi ameunga mkono kauli iliyotolewa jana na Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (COSAFA) kupinga ubaguziwa utu na vurugu zinazoendelea nchini Afrika kuelekea kwa michuano ya COSAFA. Katika kuunga mkono kauli hiyo, Malinzi amemwandikia barua Rais wa COSAFA Seketu Patel na nakala yake kwenda kwa Dr. Danny Jordan Rais wa Chama cha Mpira nchini Afrika Kusini (SAFA) akielekeze masikitiko yake juu ya mauaji na vurugu yanatokoea nchini humo. Aidha Malinzi ameeleze imani yake kuwa, kwa kushirkiana kwa pamoja nchi za Kusini mwa Afrika zitaweza kuutumia mchezo wa mpira wa miguu kama kiunganishi cha vijana, na kipaza sauti cha kuhamasisha utokomezaji wa ubaguzi wa uraia wa mtu. Mapema jana Rais wa COSAFA, Seketu Patel alisema nchini Afrika Kusini baadhi ya miji kumekua na taarifa ubaguzi, vurugu na kutokea mashambulio zinazofanywa ili kuwataka wageni waondoke nchini humo, ila wao kama COSAFA wamepanga kuitumia michuano hiyo kama sehemu ya kurejesha amani na utulivu kwa wakazi huko. COSAFA ni michuano inayojumuisha watu kutoka katika mataifa mbalimbali, kuelekea kwenye michuano hiyo sie tupo nyuma ya SAFA kuhakikisha michuano hiyo inafanyika na kurejesha amani na utulivu, kuwafanya watu wote kuungana na kuwa kitu kimoja "alisema Patel" Michuano ya COSAFA inatarajiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu katika jimbo la Kaskazini-Magharibi (North-West Province) ambapo hakujaathirika na mashambulio hayo, na serikali ya Afrika Kusini imesema itahakikisha ulinzi na usalama unaendelea kuwepo na kuimarika kwa hali ya juu. Chama cha Soka nchini Afrika Kusini (SAFA) kimelaani vurugu hizo zinazoendelea nchini humo na kusema wao kama wenyeji wamejiandaa kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa amani na usalama, hata wakati wa Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini (2010), palikua na tishio la hali ya usalama lakini michuano iliweza kufanyika na kumalizika kwa usalama. Aliyekua Rais wa Chama cha Soka cha Nambia (NFA) John Muinjo, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa COSAFA na mjumbe wa muda mrefu amesema anaamini michuano hiyo itarudisha umoja kwa watu wanaoishi nchini Afrika Kusini. Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17, 2015 katika jiji la Rusternburg (North-West Province) nchini Afrika Kusini katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng ikishirikia nchi za Botswana, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, South Africa, Swaziland, Zambia and Zimbabwe. Nchi za Ghana na Tanzania zinashiriki michuano kama nchi waalikwa.

    No comments:

    Post a Comment