JOHANNESBURG – Chama cha soka cha Afrika ya Kusini(Safa)kimetangaza kikosi cha Bafana Bafana kitacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya nchi mbili jirani,katika kuonyesha kupinga vitendo vya mashambulizi dhidi ya wageni yanayoendelea nchini humo. Safa kimesema mashambulizi hayo yameharibu taswira ya Afrika Ya Kusini. Bafana Bafana,Banyana Banyana na timu zote za vijana pamoja na zile zote za taifa hilo zimelaani mashambulizi hayo. Hata hivyo Safa bado hawajasema ni timu zipi zitacheza dhidi ya Afrika Ya Kusini katika michezo hiyo ya kampeni ya kupinga mashambulizi ya kifedhili dhidi ya raia wa kigeni nchini humo. Mashambulizi mbalimbali yamelipuka kwa siku za karibuni,yakianzi kwenye mji wa KwaZulu-Natal na kusambaa hadi kwenye mji wa Johannesburg pamoja na vitongoji vyake. Rais Jacob Zuma aliamua kusitisha safari yake ya kuelekea nchini Indonesi katika dakika za mwisho hapo majuzi ili kukabiliana na masaibu hayo,na mapema majuzi aliweza kuzungumza na maelfu ya wageni ambao wameyakimbia makazi yao katika jiji la Durban.
No comments:
Post a Comment