• Breaking News

    Wednesday, 5 October 2016

    WATUMISHI 3 WASIMAMISHWA KAZI



    Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo,
    amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa
    tuhuma za ubadhilifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015. 
    Na Mwandishi wetu,
    Watumishi hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae
    alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfuta  cheo hicho,bwana Evansi Mwalukasa alikuwa
    mwekahazina wa halmashauri na  bwana Sembeli
    Sinayo yeye alikuwa mwanasheria wa halmashauri.
    Maamuzi hayo yamefikia baada yakubainika kuna
    upotevu  wa fedha za uchagu takribani Milioni
    188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa
    wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata
    taratibu za manunuzi ya serikali.
    “Kuanzi sasa nawasimamisha  kazi hawa watumishi watatu kwasababu
    wameisababishia serikali hasara ya takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha
    za uchaguzi”.
    Aidha Muheshimiwa Gambo alisema maamuzi hayo
    yametokana na taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda yakuchunguza mapato
    na matumizi ya fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi
    ambazo zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
    Ambapo fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi
    ambayo hayakufuata taratibu na sheria za manunuzi ya serikali ,hivyo ni kinyume
    kabisa na taratibu za serikali katika maswala ya manunuzi.
    Akisisitiza kwa watumishi wa serikali kufuata
    taratibu, sheria na kanuni mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ili
    kuepuka migongano na uvunjifu wa sheria mahala pa kazi nakupelekea kupoteza
    kazi  zao.
     
    Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Ngorongoro wakimsikiliza Mkuu wa
    Mkoa (hayupo pichani),alipokuwa akizungumza nao baada yakufanya ziara
    katika ofisi za halmashauri hiyo, Wilayani Ngorongoro.

    No comments:

    Post a Comment