NA HERIETH SEMGAZA
Jeshi la Police Kanda Maalum Dar es salam limesema matukio ya kiuhalifu jijini humo yameanza kupungua hii ni kutokana na kutumia mbinu ya ulinzi shirikishi linaloundwa na kiongozi wa serikali za mitaa kwa kusaidiana na police kadhaa,ili kupunguza uhalifu.
Hayo yamesemwa na Kamishina wa Police Kanda Maalumu ya Dares salaam Kamanda Simon Sirro mkutano na waandishi wa habari kituo cha kati jijini Dar es salaam wakati alipotaja idadi ya matukio yaliyojitokeza hivi karibuni jijini humo.
Kamanda Siro amesema jeshi hilo limesikitishwa na uharibifu uliojitokeza siku ya tarehe 2 /10/2016 katika uwanja wa taifa ,nakueleza kuwa watafanya uchunguzi ili kubaini watu wote walioshiriki katika uharibifu huo na kuwafikisha mahakamani mara tu wanapokamatwa.
Kamanda Siro ameongeza kuwa jeshi la police kanda maalumu ya Dar es salaam kupitia kikosi cha usalama barabarani kimekamata makosa mbalimbali kuanzia tarehe 27/9/2016 hadi tarehe 2/10/2016 na kuingizia serikari kiasi cha jumla ya tozo Tsh 464,790000/=
Pamoja na hayo amewaomba wananchi kuwa wepesi kutoa taarifa za kiuhalifu bila woga pindi wanapoziona au kusikia ili jeshi la polisi liendelee na kazi kubwa ya kudhibiti na kutokomeza uhalifu jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment