SHIRIKA la Shina Inc la nchini Marekani na Tanzania,limetambulisha blanketi la kuulia wadudu wasumbufu na wale wanaosambaza maradhi kama mbu, chawa na kunguni.
Katika utambulisho huo, rais wa shirika hilo nchini Marekani na Tanzania, Jesca Mushala alisema kuwa kama mtanzania akiwa nje ya nchi yake aliona kitu hicho kuwa ni kizuri ndio maana akafanya jitihada ili kiweze kuwasaidia watanzania waishio kwenye maeneo yenye wadudu hao hususani mbu.
alisema mablanketi hayo yamethibitishwa kwa majaribio mbalimbali kuwa ni salama kwa binadam, hivyo kwa hapa nchini wamekuja na blanketi 1100 kwa ajili ya kusambaza kwa ajili ya majaribio na kupata mrejesho.
"Mablanketi haya yanakinga mbu, yanaua mbu, kukiwa na joto yanaleta baridi, kukiwa na baridi yanaleta joto. pia wadudu wengine wanaonyonya damu wakiwemo kunguni na kiroboto wanakufa," alisema.
Alisema hapa nchini wameanzia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Kagera, Pemba na Unguja na baada ya hapo wataangalia mrejesho watakaoupata kabla ya kusambaza nchi nzima.
Aliongeza kuwa juu ya blanketi hilo mbu hawezi kuruka juu ya futi tano kwenye blanketi hilo. alisema matumizi yake ni kujifunikia wakati wa kulalia ama ukiwa unatembea.
Blanketi hilo lina teknolojia ya kisasa, utafiti wake umefanywa kwa miaka 25 kabla ya kuanza kutumika. zinatumika kwa nchi 40 duniani.
baaada ya hapo shirika hilo niaendelea kutoa misaada kwa vijiji mbalimbali kama vile kisarawe na sehemu nyenginezo mambazo zipo mbali na dar es salaam na pwani wana kijijinn cha kisarwe walifurahi kwa hudumma hilo na kutilia mkazo kwa kutoa burudani ya maigizo na kuimiza serikali kuwaunga mkono kwa jambo hilo zuri
No comments:
Post a Comment