• Breaking News

    Tuesday, 4 October 2016

    Kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu kuzalisha lita milioni 2 kwa mwaka.


    Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha  wakati makamu uyo alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Kushoto kwa makamu wa Rais wa Cuba ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee  na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.
    vid2
    Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha Biotec Product ambacho kinazalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria Bw.Alejandro Torres kilichopo Mkoani Pwani.
    vid3
    Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Dkt Samuel Nyantahe akizungumza jambo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa katika kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.
    vid4
    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha  akizungumza jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa wakati makamu uyo alipotembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Katikati ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee  na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.
    vid5
    Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisisitiza jambo wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Kulia kwake ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee  na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha  na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
    vid6
    Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa Mhe.Salvador Valdes Mesa(kushoto) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee  na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(katikati) wakimskiliza Meneja Teknolojia wa kiwanda cha Biotec Product Bi.Lourdes Gonzalez kinachozalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.
    Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
    ………………………………………………………….
    Na Daudi Manongi,MAELEZO
    Kiwanda cha Biotec Product kilichopo kibaha mkoani Pwani ambacho kinamilikiwa kwa ubia baina ya Serikali za Tanzania na Cuba kimekusudia kuzalisha lita milioni 2 za dawa za viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa malaria nchini.
    Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto  Mhe.Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa katika kiwanda hicho.
    “Kiwanda hiki kitasaidia katika vita yetu ya kupambana na malaria kwa kuwa ni miongoni mwa  magonjwa yanayowasumbua  Watanzania na Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kuwatibu wagonjwa” alisema Waziri Ummy
    Waziri Ummy alisema dawa zinazotengenezwa kiwandani hapo zitaisadia tatizo hili na sekta ya Afya kwa kuwa uwezo wa Serikali ni kuzalisha lita milioni 2.5 kwa mwaka na wakati kiwanda hicho kinaweza kuzalisha lita milioni 2 kwa mwaka.
    Kwa mujibu wa Waziri Ummy alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa katika Watanzania 100, watanzania 14 wanapatwa na ugonjwa wa malaria.
    Aliongeza kuwa dawa hizo zina uwezo kuua viuadudu hivi katika hatua za mwanzo za kuzaliwa kwa mbu na hivyo uzalishaji huo utapoanza utasaidia kupunguza gharama za kutibu malaria, kununua vyandarua na  dawa za kuua wadudu wa mbu.
    Aidha Sekta ya Afya na Halmashauri zote nchini zitawajibika kununua dawa katika kiwanda hiki kwa sababu wao ndo wadau wakubwa wa sekta hii.
    Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Dkt Samuel Nyantahe alisema dawa zitazozalishwa kiwandani hapo zitauzwa katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima.
    Akifafanua zaidi alisema Serikali ya Cuba imekubali kusaidia katika kutafuta masoko na hivyo wanategemea kujenga viwanda vingi vya aina hiyo  ili kufanikisha adhma ya Serikali  ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.
    Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema Mkoa huo  umejipanga kuwa mkoa wa viwanda kwa kuwa una ardhi ya kutosha, na pia kiwanda hicho kinatarajia kutengeneza ajira kwa wananchi na hivyo  kuwataka wawekezaji kuwekeza katika viwanda

    No comments:

    Post a Comment