• Breaking News

    Friday, 2 September 2016

    Wasiosoma elimu ya juu walia kudaiwa mikopo



    BAADA ya serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoa orodha ya majina ya wadaiwa sugu wa mikopo hiyo, kumeibuka taharuki kwa baadhi ya watumishi wilayani Namtumbo, Ruvuma baada ya kuingizwa kwenye orodha hiyo huku baadhi yao wakidai hawajasoma elimu ya juu au kuhusika na kuomba mkopo huo.
    Ofisa Habari wa Wilaya ya Namtumbo, Yeremias Ngerangera alithibitisha kupokea malalamiko ya walimu sita wa shule za msingi ambao wanadai hawajasoma elimu ya juu wala kuomba fedha hizo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
    Ngerangera aliwataja walimu waliowasilisha malalamiko kuwa ni Thomas Komba anayedaiwa Sh milioni 3.4, Joseph Chengula anayedaiwa Sh milioni 12.9 na Michael Haule anayedaiwa Sh milioni 2.7.
    Aliwataja wengine kuwa ni Michael Jimmy anayedaiwa Sh milioni 29.1, Deogratias Haule anayedaiwa Sh milioni 16.0 na Marry Haule anayedaiwa Sh milioni 2.6 ambao wanailalamikia bodi kuwadai fedha hizo wakati hawajakopa wala kusoma kwa fedha za bodi hiyo.
    Hata hivyo, Ngerangera alisema Halmashauri ya Wilaya Namtumbo inaendelea kupokea malalamiko hayo ya walimu kwa maandishi ili kuwasilisha Bodi ya Mikopo kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kubaini ukweli wa madai hayo.
    Mwalimu Komba na Chengula, walifika katika ofisi ya Ofisa Habari wa Wilaya ya Namtumbo kuelezea masikitiko yao juu ya kuingizwa kwenye madeni ya wadaiwa sugu wakidai hawajasoma elimu ya juu wala hawajawahi kuomba mkopo huo.
    Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo imewataka walimu wengine tisa kuwasilisha vielelezo vyenye kuonesha ushahidi kwamba hawakusoma elimu ya juu wala kuomba mkopo huo na wale ambao wanadai kuwa wamemaliza madeni yao pia nao wawasilishe ushahidi wao kwa Ofisa Utumishi, John Mpangala ili upelekwe Bodi ya Mikopo kwa uchunguzi wa madeni hayo.
    Katika siku za karibuni, Bodi ya Mikopo ilitangaza majina ya wadaiwa wake sugu kwa nia ya kuhakikisha kuwa wanafahamika na wanabanwa kurejesha fedha walizotumia kusomeshwa ili zisaidie kusomesha wanafunzi wengine.
    Juzi mjini Dodoma, wabunge kadhaa walisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mikopo kuirejesha kwa hiari ili kuiwezesha bodi kukopesha wanafunzi wengi

    No comments:

    Post a Comment