Pichani wa pili kutoka kushoto mwenye suti nyeusi ni DC. Mhando akiwahoji wavamizi wa Ardhi ya wananchi wa Kijiji cha Kabage.
…………………………………………………..
Takribani Hekali 501 zimerudishwa mikononi mwa wananchi wa kijiji cha Kabange kata ya Sibwesa wilaya mpya ya Tanganyika mkoani Katavi baada ya kushikiliwa na wavamizi wa kikundi cha Nguvu kazi Group kwa miaka 9 sasa waliolivamia eneo la bonde la kijiji hicho kwa kutumia nyaraka za kugushi na kulitumia eneo hilo kwa ajili ya kilimo cha zao la mpunga
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando kwenye kikao cha ndani kilichofanyika katika shule ya msingi Kabage mara baada ya kutembelea eneo hilo lenye mgogoro kwa miaka 9 hali iliyopelekea vifo vya wananchi zaidi ya 6 katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita kwa ajili ya kugombania Ardhi.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhuria katika kikao hicho wameipongeza Serikali kwa kutatua mgogoro huo huku wakieleza kuwa waliishi pasipo kuwa na amani kwa kuhofia maisha yao.
Aidha kwa Upande wake Afisa Ardhi wa wilaya ya Tanganyika Bwana Mussa Yohana amewataka wananchi kufuata sheria za kumiliki Ardhi kihalali ili kuepusha migogoro ambayo imekuwa kero katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo.
Nae katibu wa kikundi cha Nguvu kazi group Ramadhani Kasonso akiongea mbele ya wananchi wa kijiji hicho mara baada ya kuamriwa kurudisha Ardhi kwa wanakijijii amewaomba kusahau yaliyopita na kuendeleza ujenzi wa taifa huku akiomba uongozi wa kijiji hicho kulipa Trekta ya kulimia mali ya Nguvu kazi Group ambayo ilichomwa moto na wananchi kutokana na mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment