TANZANIA ni miongoni mwa mataifa 13 ya Afrika Mashariki yaliyokubaliana na kuweka saini tamko la pamoja la mataifa hayo kuendelea kushirikiana kwa karibu kupambana na dawa za kulevya na makosa mengine ya jinai.
Hatua hiyo imefikiwa katika mkutano wa pamoja wa uzinduzi wa mpango kazi wa kikanda wa Umoja wa Mataifa (UN) wa kudhibiti dawa za kulevya na makosa mengine ya jinai (UNODC) wa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2021, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya Agosti 29 mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome, ambaye aliiwakilisha Tanzania katika uzinduzi huo alisema ulihusisha uwekaji saini wa tamko hilo la pamoja la mataifa hayo kuendeleza mapambano dhidi ya dawa za kulevya na makosa mengine ambayo ofisi ya UN inawajibika nayo.
Alisema malengo ya mpango kazi huo yanakwenda sambamba na dhamira na malengo ya serikali ya kupambana na uovu ikiwemo dawa za kulevya, rushwa, usafirishaji haramu wa binadamu na vitendo vya ugaidi.
“Huu mpango kazi ni mzuri na unahusisha maeneo mbalimbali ya changamoto ambazo Tanzania imekuwa ikikabiliana nazo kama dawa za kulevya, rushwa, usafirishaji haramu wa binadamu na vitendo vya kigaidi ,” alisema.
Alisema taifa linalohitaji maendeleo kwa haraka halina budi kuwa la kwanza katika kuuchangamkia mpango huo. Aliyataja mataifa hayo mbali na Tanzania kuwa ni Burundi, Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Visiwa vya Shelisheli, Somalia na Uganda ambayo yalishiriki uzinduzi huo.
Profesa Mchome alisema lengo ni kuunga mkono na kuimarisha uwezo wa mataifa haya kudhibiti na kupambana na vitendo vya aina hiyo, udhibiti wa rushwa ikiwa na lengo la kuendelea kuimarisha uwezo wa mataifa haya katika utekelezaji wa Mkataba wa Ummoja wa Mataifa Dhidi ya Rushwa.
“Nguzo ya tatu ni kuhusu kuzuia ugaidi ambapo lengo litakuwa ni kuendelea kuunga mkono na kuimarisha mifumo ya kitaifa ya makosa ya jinai ili kuiwezesha kumudu na hivyo kukabiliana ipasavyo na tishio la ugaidi ambao unaendelea
No comments:
Post a Comment