• Breaking News

    Wednesday, 31 August 2016

    TWEET- SHABIKI NGULI WA ARSENAL AKIRI KUTOMTAMBUA STRAIKA MPYA PEREZ

    1
    1Lucas Perez tayari amemalizana na Arsenal na kutua klabuni hapo kwa ada ya paundi mil 17 akitokea klabu ya Deportivo La Coruna. Anatarajiwa kutoa ushindani mkubwa kwa straika wa sasa Olivier Giroud.
    Mashabiki wa Arsenal wanaweza kuwa walikuwa na ndoto za kuwapata Antoine Griezmann au Karim Benzema, lakini Arsene Wenger ameona Perez ni mtu sahihi wa kumpa faraja kwenye safu yake ya ushambuliaji.
    Msimu uliopita, Perez alifunga mabao 17 na kutoa assists 8, takwimu ambazo si haba kwa mchezaji aliyekuwa kicheza timu yenye uwezo wa kati.
    Lakini uwezo au kiwango chake huko nchini Uhispania unaonekana kutotambulika kwa moja ya washabiki nguli wa Arsenal Piers Morgan.
    Morgan, ambaye anasifika kwa kutumia mtandao wa Twitter mara nyingi kumkosoa vikali kocha Arsene Wenger pale anapoenda kinyume na matarajio ya washabiki wa timu hiyo, hakuwa nyuma kutoa comment kwenye usajili huu wa Perez 

    No comments:

    Post a Comment