• Breaking News

    Wednesday, 10 August 2016

    RC AZUIA TOZO DAR

    MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapiga marufuku mawakala wanaotoza faini za kuegesha magari vibaya katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo hadi hapo yatakapotengenezwa maeneo rasmi kwa ajili ya maegesho ya magari.
    Makonda alitoa kauli hiyo jana wakati alipofanya ziara kujionea hali halisi ya kituo hicho.
    Alisema haiwezekani mawakala wakaendelea kutoza faini za maegesho ambayo si sahihi wakati katika eneo hilo hakuna maeneo maalumu kwa ajili ya maegesho ya magari.
    “Nataka maeneo rasmi yakishatengwa ndipo muanze kutoza faini, mmekuwa mkiwasumbua wananchi hawajui wapi ni sehemu ya maegesho na wapi si sehemu ya maegesho wekeni alama ndipo muanze kuwatoza,” alisema Makonda.
    Licha ya kutoa kauli hiyo, Makonda pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji kabla ya kumalizika wiki hii kuhakikisha kituo hicho kinawekwa taa ili kuondoa usumbufu wanaokutana nao abiria na wananchi hasa wakati za usiku.

    No comments:

    Post a Comment