Klabu ya Leicester City ya England leo August 10 2016 imetangaza rasmi kumuongezea mkataba wa miaka minne kocha wake raia wa Italia Claudio Ranieri, Leicester Citywamemuogezea Ranieri mkataba wa miaka minne na atakuwa na Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England hadi 2020.
Leicester City wamemuongezea mkataba Ranieri kutokana na kuipa Ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita kwa mara ya kwanza katika historia, Ranieri kaongezewa mkataba lakini ukimuuliza kama atatetea taji lake msimu huu ni gumu kwake kusema ndio.
“Hilo ni swali kugumu kujibu lakini bilashaka inawezakana kutetea taji letu na tutajaribu kufanya hivyo yaani kutetea tena Kombe letu la Ligi Kuu England”
No comments:
Post a Comment