• Breaking News

    Wednesday, 10 August 2016

    NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla amesisitiza kuwa hudum
    a zote za afya za magonjwa anayowapa watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini ni bure.
    Alisema ikitokea mwenye mgonjwa anatakiwa kulipia, mhusika atoe taarifa mahali panapohusika.
    Dk Kigwangalla alisema hayo jana jijini Dares Salaam wakati akizungumza katika uzinduzi wa ripoti inayohusu upatikanaji wa huduma za afya na wahudumu kuongezeka kwa mwaka 2015. Ripoti hiyo ilitokana na utafiti ulioandaliwa na mradi wa sauti za wananchi chini ya Taasisi ya Twaweza.
    Alisema kupitia Sera ya Afya nchini, watoto ni moja ya kundi la wahitaji wa matibabu bure, wengine wakiwa ni wazee zaidi ya miaka 60 na wote wenye kipato cha chini ambao hawapaswi kutozwa gharama.
    Kuhusu madai ya kuwepo kwa uhaba wa upatikanaji wa dawa za wanaoishi na virusi vya Ukimwi, Dk Kigwangalla alisema taarifa hizo si za kweli kwani upo uhakika kuwa ipo akiba ya dawa kwa miezi sita kwenda mbele kwa Jiji la Dar es Salaam huku katika mikoa mingine uhakika wa upatikanaji wa dawa hizo ukiwa ni wa miezi mitatu mbele.
    Alisema kinachoweza kukosekana ni dawa za magonjwa nyemelezi lakini serikali imekuwa makini sana kufuatilia uwepo wa dawa hizo pamoja na za magonjwa mengine ambayo ni magonjwa sugu.
    Kuhusu kuwepo kwa makundi yanayolipia huduma hizo ilhali zinatolewa bure, Dk Kigwangalla alisema Sera ya Afya Tanzania iko wazi kwamba magonjwa mbalimbali ambayo ni sugu yako katika msamaha wa kulipiwa. Alisema kinachojitokeza ni baadhi ya vifaa vinavyotakiwa kuwepo katika stoo za vituo vya huduma za afya kutokuwepo kwa wakati

    No comments:

    Post a Comment