Kanda ya video mjini Paris ilioonyesha mkahawa mmoja ukikataa kuwahudumia wanawake wawili Waislamu imezua hisia kali nchini Ufaransa.
Katika kanda hiyo,iliosambazwa sana katika mitandao ya kijamii ,mwanamume anamwambia mwanamke aliyevaa Hijab :''Magaidi ni Waislamu na Waislamu wote ni Magaidi''.
Kisa hicho kilitokea katika mkahawa wa Le Cenacle,Tremblay-en-France siku ya Jumamosi usiku.
Siku ya Jumapili,mtu huyo aliomba msamaha kwa kundi lililokongamana nje ya mkahawa huo.
Anasema kuwa alijisahau na kutoa matamshi hayo kutokana na mjadala unaoendelea nchini humo kuhusu vazi la Burkini katika fukwe za bahari za Ufaransa,na kwamba ana rafikiye aliyefariki katika shambulio la mjini Paris katika eneo la Bataclan mnamo mwezi Novemba.
No comments:
Post a Comment