SIKU moja kabla ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, haijaingia katika historia ya kisayansi duniani ya kuwa mwenyeji wa tukio ya kupatwa na jua, maandalizi ya kushuhudia tukio hilo wilayani humo yamekamilika kwa kiasi kikubwa cha kuwawezesha Watanzania wapatao 500 kushuhudia tukio hilo.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza Tanzania kutokea tukio hilo tangu Aprili 18, 1977 na kwamba tukio kama hilo la kihistoria linatarajiwa kutokea tena nchini Mei 21, 2031.
Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi Teknolojia na Elimu ya Mazingira kutoka Chuo Kikuu Huria chaTanzania (OUT), Dk Noorali Jiwaji amesema tayari serikali ya wilaya hiyo imetoa eneo linaloonesha anga lote kwa ajili ya kuangalia tukio hilo.
Kwa habari zaidi soma toleo la HabariLEO kesho
No comments:
Post a Comment