• Breaking News

    Monday, 29 August 2016

    BODI YA FILAMU YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA WADAU WA FILAMU

    FIL1
    Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Waandishi wa Miswada ya Filamu kwa baadhi ya waandishi hao leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu MFIL1wenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Miswada ya Filamu Tanzania (TASA) Haji Jumbe.
    FIL2
    Mwandishi wa Script kutoka Marekani Bi. Emma Rosenbaum akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Uandishi  wa Miswada ya Filamu kwa baadhi ya waandishi hao leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na Mwanafunzi wa Utengenezaji wa Filamu kutoka Los Angels Marekani Leo Masciarelli.
    FIL3
    Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Miswada ya Filamu Tanzania(TASA) Bw.  Christian Kauzeni akisoma risala ya Chama hicho wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Waandishi wa Miswada ya Filamu kwa baadhi ya waandishi hao leo Jijini Dar es Salaam.
    FIL4
    Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Miswada ya Filamu Tanzania (TASA) Cheristian Kauzeni  mara baada ya kukabidhiwa fomu kwa ajili ya kujiunga na chama hicho leo Jijini Dar es Salaam.
    …………………………………………………………….
    Bodi ya filamu Tanzania imeahidi kuendeleza ushirikiano na wadau wa sekta ya filamu kuhakikisha sekta hiyo inakuwa chachu ya maendeleo nchini.
    Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Joyce Fissoo wakati akifungua mafunzo ya uandishi wa miswada ya picha jongefu kwenye ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO leo jijini Dar-es-salaam.
    Mafunzo hayo ya siku nne yamewezeshwa kwa ushirikiano kati ya Bodi ya Filamu Tanzania na Chama cha Waandishi wa Miswada ya Picha Jongefu Tanzania (TASA).
    Kwenye hotuba yake Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo alisisitiza umuhimu wa mswada kwenye utengenezaji wa filamu pale aliposema “mswada ni msingi wa filamu yoyote na mswada bora ndio utakao kuhakikishia filamu bora”.
    Aidha ameupongeza uongozi wa Chama wa Waandishi wa Miswada ya Filamu Tanzania kwa kuandaa mafunzo hayo ambapo ameonyesha imani yataleta mabadiliko chanya kwenye ubora wa filamu za ndani. Mbali na kuwapongeza viongozi wa chama hicho pia aliahidi kutoa ushirikiano wakati wowote atakapohitajika ili kuboresha tasnia ya filamu ncini. Kutekeleza kwa vitendo ahadi hiyo Fissoo alikubali kuwalipia ada ya uanchama washiriki wanane ambao walikuwa bado hawajajisajili kwenye chama hicho.
    Mafunzo hayo ya siku nne yatakuwa ya vitendo na shirikishi ambapo yataongozwa na wakufunzi wawili kutoka nchini Marekani na yana lengo la kuwaongezea ujuzi waandishi wa miswada ya filamu wapatao 65 ili waweze kuandika miswada yenye ubora wa kimataifa.
    Takwimu za Bodi ya Filamu Tanzania zinaonyesha jumla ya miswada 33 iliwasilishwa mwaka wa fedha 2014/2015 kati ya jumla ya filamu zaidi ya 1400 zilizokaguliwa. Idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na maombi 169 yaliyowasilishwa ndani ya mwaka huo kutoka kampuni za nje ambapo mamombi yote sawa na asilimia 100 yaliambatanishwa na miswada yake.
    Kwenye risala yake Katibu wa TASA Christian Kauzeni alizitaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo wanachama wao ni pamoja ukosefu wa sera ya filamu, wanachama kushindwa kujua wajibu wa mamlaka zinazosimamia sekta ya filamu kama vile COSOTA, Bodi ya Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)na kukosekana kwa mfumo yakinifu wa elimu kwa waandishi wa miswada ya filamu. Bi. Fissoo aliahidi kuzishughulikia changamoto hizo

    No comments:

    Post a Comment