• Breaking News

    Tuesday, 30 August 2016

    Bodi inayochunguza viwango vya filamu Kenya kuchunguza ''kipindi cha ngono''


    Waandaaji Kaz na NiniImage copyrightTHE SPREAD
    Image captionWaandaaji Kaz na Nini hutangaza kipindi hicho kila Ijumaa kuanzia saa sita mchana
    Bodi inayofuatilia inayofuatilia ujumbe wa filamu nchini Kenya imeonya kwamba itachukua hatua dhidi watengenezaji wa vipindi vya mazungumzo ya ngono ,vilivyozinduliwa mwezi Aprili, ikiwa uchunguzi utabaini kwamba wamekuwa wakivunja sheria.
    Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Filamu ya kenya Ezekiel Mutua inahusu kipindi kinachofahamika kama " cha kwanza cha wapnzi wa jinsia moja wa kike cha TV kinachoongozwa na wapenzi wa jinsia moja maarufu wa kike ".
    Taarifa hiyo imeongeza kuwa kipindi hicho, Kinachoitwa ''The Spread Podcast," kilitarajiwa kusambazwa na televisheni ya WGNTV, Iliyopo kwenye mtandao wa dunia wa internet unaopatikana nchini Kenya".
    Amesema yale yanayozungumziwa kwenye kipindi hicho yana uwezekano mkubwa wa kuwa kinyume na sheria ya nchi inayopiga marufuku mapenzi ya jinsia moja na suala zima la kuyanadi.
    Bw Mutua aliwahi kutoa wito wa kupigwa marufuku kwa kipindi hicho kwa ''kutotokuwa na cha maadili'' na "kukiuka sheria".

    No comments:

    Post a Comment