Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo umekutana na Uongozi wa klabu ya Simba SC ukiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Collin Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano akiandamana na Uongozi wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA). Kikao hiki kiliitishwa na TFF kujadili utata wa kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.
Katika kikao cha leo pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.
Kwa pamoja pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.
TFF imevitaka vilabu kushirikiana na SPUTANZA na Bodi ya Ligi katika kuweka mifumo mizuri ya uingiaji mikataba. TFF inao mkataba mama (template) ambao vilabu vyote na wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa mikataba yao (individual contracts between players and clubs). Aidha TFF imewataka wachezaji kuelewa mikataba kabla ya kutia sahihi.
TFF itazidi kuboresha mfumo wa usajili wa wachezaji na mikataba ili kuweka mazingira sawia kati ya pande zote mbili (Wachezaji na vilabu)
Makubaliano yamefanyika leo tarehe 9 Juni 2015 na kusainiwa na:-
- Collin Frisch - Simba SC
- Ramadhan Singano - Mchezaji
- Mussa M. Kissoky - SPUTANZA
- Mwesigwa J. Selestine - Katibu Mkuu - TFF
No comments:
Post a Comment