Meneja mpya wa klabu ya Real Madrid Rafael Benitez amewaambia waandishi wa habari kuwa anavutiwa na mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling.Benitez aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kumtambulisha kama meneja mpya wa Real Madrid mbele ya waandishi wa habari.
Meneja huyo wa zamani wa Liverpool amemaliza misimu miwili na timu ya Napoli,na kujiunga na timu ya Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitatu katika timu hiyo inayotumia uwanja wa Bernabeu huku akitoa ahadi’’Soka lenye ubora’’ambalo’’litawafanya kutwaa makombe’’
Wakati alipoulizwa juu kuhusiana na Sterling mchezaji wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 20,Benitez alisema’’Tunavutiwana Raheem,hili siyo siri-lakini siyo moja ya wachezaji wetu kwa hiyo siwezi kumzungumzia zaidi.’’
No comments:
Post a Comment